Header Ads

http://mtafitiblog.blogspot.com/p/blog-page.html

Nyalandu: Nimeliona tabasamu la Lissu, tuendelee kumuombea





Baada ya kukaa hospitali kwa zaidi ya mwezi mmoja Lissu akipatiwa matibabu, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amekiri kuona tabasamu la Mbunge huyo aliyepigwa risasi mwezi uliopita na kuwataka watanzania waendelee na maombi.
Kupitia mtandao wake wa Instagram Nyalandu amesema kwamba shauku aliyonayo Lissu ndani ya moyo wake ni kuiona siku iliyo njema pia kufurahia siku kila asubuhi.
Nyalandu ameandika “Tuendelee kumwombea ndugu yetu Tundu Lissu. Nimeliona tabasamu la uso wake leo, na hakika Mungu anaendelea kujibu maombi ya Watanzania, na wote wanaomkumbuka katika sala na dua zao katika majira na saa hii ya kujaribiwa kwake” ameandika Nyalandu.
“Tusimame pamoja naye, kwa kuwa shauku ya moyo wake ni kuiona siku iliyo njema, aweze kuifurahia kila asubuhi kama apendavyo Mungu”ameongeza.
Lissu alipigwa risasi na watu wanaodaiwa kuwa wasiojulikana tangu Septemba 07 akiwa mjini Dodoma nje ya nyumba yake alipokuwa ametoka Bungeni kutekeleza majukumu yake na sasa bado yupo hospitali ya Nairobi nchini Kenya akiendelea na matibabu.

No comments

Powered by Blogger.