JWTZ WAANZA KAZI MERERANI
JESHI la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) limeanza kutekeleza agizo la Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dk John Magufuli aliyelitaka kujenga uzio wa kuzunguka kitalu A hadi D katika eneo madini ya tanzanite, Mirerani Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara ili kudhibiti uchimbaji na biashara ya madini hayo.
Dk Magufuli juzi aliiagiza JWTZ kwa kushirikiana na Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa (Suma JKT) kuanza mara moja kujenga uzio kwenye eneo la kitalu A hadi D lililopo eneo la Simanjiro ambalo kunapatikana madini ya kipekee ya tanzanite. Aidha, aliagiza kufungwa kwa kamera maalumu, kuweka fensi maalumu na kutakuwa na eneo moja la mlango wa kutokea na kuingia ili kubaini wezi wanaoiba madini hayo.
Jana, Meja Jenerali Michael Isamuyo akiwa na wataalamu wa JWTZ, wamefika Mirerani kwa helikopta na kisha kukagua eneo lenye vitalu vya tanzanite wakiwa angani na baadaye wakatua na kukagua wakiwa ardhini kwa kutumia magari na kutembea kwa miguu. Akizungumza baada ya kutua kwenye uwanja wa wazi wa Mererani, Meja Jenerali Isamuyo alisema JWTZ imeanza kutekeleza agizo la Rais na Amiri Jeshi Mkuu mara moja na ipo tayari kukamilisha kazi kama ilivyokusudiwa.
Meja Jenerali Isamuyo alisema baada ya kutembea kwa miguu katika eneo la vitalu A hadi D, amebaini kuwa eneo linalopaswa kujengwa uzio huo ni la kawaidana ametaka wananchi watoe ushirikiano wa kutosha wakati wa ujenzi wa uzio huo. Alionya kuwa wakati wa utekelezaji wa jukumu hilo, JWTZ haitarajii kukwamishwa na mtu yeyote na haitakuwa tayari kukwamishwa kwa namna yoyote. Baadhi ya viongozi wa Chama cha Wachimbaji wa Madini wa Mkoa wa Manyara waliokuwepo wakati Meja Jenerali Isamuyo akitua na akikagua eneo la vitalu vya tanzanite, walimpongeza Rais Magufuli kwa kuagiza kujengwa kwa uzio huo na wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha wakati wa ujenzi huo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Manyara, Hamis Kim maarufu Komandoo na Katibu wa Wachimbaji Tawi la Mirerani, Aboubakar Madiwa walisema uzio huo utasaidia kuokoa mapato na utoroshaji wa Tanzania ambao umekuwa ukisababisha Tanzania kupoteza mapato makubwa. Aidha, Katibu Mkuu wa chama hicho, Curtius Msosa na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Mirerani, Wariamangi Sumari wamepinga kauli iliyotolewa na mwenyekiti wao aliyenukuliwa na gazeti moja la kila siku akitoa kauli za kupinga ujenzi wa uzio huo na kusema hiyo ni kauli yake binafsi na siyo kauli ya chama.
Katika hatua nyingine, wauzaji, wanunuzi na wachimbaji wa madini ya tanzanite jijini Arusha wamempongeza Rais Magufuli kwa uamuzi aliochukuwa wa kuzungushia ukuta katika machimbo hayo, wakieleza kuwa uamuzi huo utalinufaisha Taifa. Mmoja wa wafanyabiashara wa tanzanite, Joackim Laizer alisema uamuzi huo unaweza kuisadia nchi kunufaika na madini hayo kwani kila mchimbaji na muuzaji wa madini atalipa kodi stahili kwa kile alichozalisha kutoka katika mgodi wake.
Laizer alisema wazo hilo liliwahi kutolewa miaka mingi iliyopita na wachimbaji wa madini hayo na wauzaji, lakini utekelezaji wake ulikuwa mgumu kutokana na kuingizwa suala hilo na siasa na kufanya nchi kukosa kodi bila ya sababu za msingi. Alimsifu Rais kwa uamuzi aliochukua kulinda rasilimali za nchi na jitihada hizo ziendelee katika rasilimali zingine ili nchi ijiendeshe bila ya kusubiri misaada kutoka nje ya nchi.
Naye Japhet Shoo maarufu kwa jina la Kidevu, alisema wenye kufanya biashara ya magendo ni wafanyabiashara wenye asili ya Kiasia kwani ndiyo mabingwa wa biashara haramu ya kuvusha madini nje ya nchi. Shoo aliitaka serikali hususani Wizara ya Nishati na Madini kuhakikisha inafanya majukumu yake ikiwa ni pamoja na kudhibiti biashara haramu inayofanywa na raia hao waliojazana jijini Arusha ambao wengi wao hawana
Titanium Oxide and Titanium Oxide sunscreen - TITONIC
ReplyDeleteTITONIC SUNSET titanium athletics - The t fal titanium sunscreen, formulated as a UV-protectant, also gives titanium stronger than steel a UV-contaminated viscosity, a chemical that's titanium price per ounce been used to 2020 ford ecosport titanium