KIBITI HAWAKUJA WAZUNGU KUCHUNGUZA
Baada ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kusikika wakidai vyombo vya usalama kutoka nje ya nchi vije kufanya uchunguzi wa shambulio la MbungeTundu Lissu, Msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas amehoji watu wangapi wamekufa wilayani Kibiti na wazungu hawakuja kuchunguza.
Dkt. Abbas Kupitia ukurasa wake wa twitter amehoji kwa kuandika “Waje wazungu? Wamekufa watu wangapi Kibiti hatukuita wazungu?Lakini hatujui pia hata hao wazungu kwao makosa ya jinai pia yamewazidi nguvu?
Aidha, Dkt Abbas ameongeza kuwa tabia ya kutuhumiana kunapotokea kosa la jinai ambalo limetendwa kwa mtu yoyote au mwanasiasa siyo vizuri kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha mtu mwenyewe akawa mshukiwa namba moja wa tukio.
“Ni busara vyombo vya dola vikaachwa vifanye kazi yake kwanza na siyo kutuhumu wakati upelelezi unaendelea kufanywa,”ameongeza Dkt. Abbas
Post a Comment