NDEGE KUTUA BABATI
U/Ndege wa kimataifa kujengwa Babati
Ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na watumishi na viongozi mbalimbali wa mkoa huo kwenye kikao cha majumuisho ya ziara yake ya siku sita mkoani Manyara.
Amesema upembuzi yakinifu ili kubaini gharama za ujenzi wa uwanja huo utafanyika mwaka 2019 na ujenzi halisi utaanza katika bajeti ya mwaka 2020/2021.
“Tumechagua eneo la Ngungungu- Mamire kwa sababu liko karibu na mbuga za wanyama; lakini pia tuna hospitali yetu kule Haydom ili kama kuna mgonjwa amezidiwa iwe rahisi kumpakia na kumpeleka kwenye hospitali za rufaa.
“Tumechagua eneo lile ili liwe ni eneo la kupumulia la Makao Makuu ya nchi Dodoma. Ikitokea kule kumejaa, itakuwa ni rahisi kwa ndege kutua hapa Babati na mtu anasafiri kwa gari na ndani ya muda mfupi atajikuta yuko Dodoma,” aliongeza.
Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewataka wakuu wa idara na wakurugenzi wa halmashauri nchini wafanye kazi kwa ukaribu na vyombo vya habari ili taarifa za kazi wanazozifanya ziwafikie wananchi kwa haraka.
“Kwenye baadhi ya wilaya kuna redio na televisheni ambazo zinaendeshwa na Halmashauri au na watu binafsi. Ni rahisi kupata nafasi ya kurusha mambo yenu mkifanyanao kazi kwa karibu. Wakuu wa idara nendeni studio mkaelezee mafanikio yaliyopatikana katika wilaya zenu na mkoa wenu kwa ujumla,” aliongeza.
Post a Comment