Beki wa ligi kuu TZ bara anayesubiri saa 24 kujua kama ataweza kuona ,
Kama ni shabiki wa soka la bongo hususani Ligi Kuu soka Tanzania bara, hakika huwezi kuzipokea kwa furaha taarifa zilizotolewa na Mbeya City kuhusu beki wake Sankhani Mkandawile ambaye ameumia katika jicho lake la kushoto baada ya kugongwa na Jacob Masawe wa Stand United wakati wa mchezo.
Taarifa iliyotolewa katika Instagram account ya Mbeya City imeeleza kuwa “Amegongwa vibaya sehemu ya nyuma ya kichwa Mahala ambapo mishipa midogo upande wa jicho la kushoto zinapita jambo ambalo limesababisha kupoteza nguvu ya jicho lake kuona”
“Tumempatia huduma ya mwanzo inabidi apumzike kwa saa 24 halafu tutapima tena kuona kama atarejea kwenye hali yake ya kawaida” Dr Guydon Makulila.
Mkandawile aliumia wakati wa mchezo dhidi ya Stand United uliyochezwa leo na kumalizika kwa sare tasa ya 0-0, hivyo taarifa ya Doctor inaeleza kuwa atalazimika kusubiri kwa zaidi ya saa 24 ili kuweza kujua kama ataweza kuona tena katika jicho lake la hilo
.
.
Post a Comment