NDALI CHAKO SHULE ZA DINI
Ndalichako ageukia ada shule za kidini
Aliyasema hayo juzi katika hotuba yake kwenye maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 25 ya Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) jijini Dar es Salaam.
Alisema baadhi ya shule hazifanani na maono ya hizo taasisi kama yanavyozungumziwa juu ya kutoa huduma ya jamii, badala yake zimekuwa za kibiashara.
“Baba Askofu (Rais wa Tume hiyo, Askofu Alex Malasusa), tuziangalie baadhi ya shule, kuna baadhi hazifanani na taasisi tunazoziongea. Katika hali ya kawaida ili shule ipate usajili inatakiwa iwe na majengo. Sasa unakuta michango hiyo ya majengo imekuwa endelevu kila mwaka mtoto analipishwa awe ameanza shule au anaendelea hii si sawa,” alisema.
Akizungumzia udahili wa wanafunzi wa elimu ya juu na kati, alisema mfumo huo ulilenga kupunguza gharama na wale ambao hawana sifa, lakini matokeo yake umekuwa ukilaumiwa na kila mtu, mwanafunzi na hata vyuo husika.
Akifafanua hilo, alisema kumekuwa na malalamiko kwa wanafunzi kuwa wamekuwa hawapangwi kwenye shule ama vyuo vile ambavyo wamevipa kipaumbele badala yake wanapangwa sehemu nyingine ambazo hawajazitaka. Ameahidi kuifanyia kazi changamoto hiyo ili tatizo hilo lisijirudie katika udahili wa mwaka 2017/18.
Awali, Askofu Malasusa aliiomba serikali kufanyia kazi matatizo yanayoikabili sekta ya elimu na taasisi za dini ili watoe huduma nzuri kwa jamii kama walivyokusudia.
Post a Comment