HICHI NDICHO KLICHOMFANYA MUIGIZAJI KUTOKA INDIA SANJAU DUTTY KUJA TANZANIA
Muigizaji Sanjay Dutt (kushoto) akipeana mkono na Mbunge Gulamali
Muigizaji mkongwe na anayefanya vizuri kwenye soko la filamu India, Sanjay Balraj Dutt, aliyekuja nchini kwa ajili ya mapumziko anatarajiwa kudumu kwa siku 21 ambapo atatembelea mbuga za wanyama na vivutio mbali mbali vilivyopo nchini.
"Uwepo wa Sanjay Dutt nchini ni fursa kubwa sana. Wahusika wa utalii hapa nchini wakiona fursa katika kuutangaza zaidi utalii wetu ni vyema pia wakamtumia kwani mtu huyu ni mkubwa sana kwenye sanaa ya filamu. Lakini pia kuja kwake hapa nchini ni wazi tunazidi kukua kwenye sekta hii, na tutapata mapato kupitia kuwepo kwake kwani atakuwepo kwa takribani siku 21" alisema Mhe. Gulamali
Hata hivyo mbunge huyo amewataka waigizaji wa filamu nchini kuchangamkia fursa ya kukutana na muigizaji huyo kwa ajili ya kupata madini yatakayowasaidia kukuza na kupanua soko la filamu.
"Huyu ni muigizaji mkubwa ningewashauri wasanii wa nyumbani wasimuachie akaondoka hivihivi.
Kama uongozi wa wassnii wa filamu wataona fursa kwake wasisite kunitafuta ili niweze kuwakutanisha naye kwani haitashindikana kutenga siku moja kwa ajili ya mazungumzo ambayo yatakuwa na faida kwenye sanaa ya nyumbani lakini kama wakiona hakuna haja basi hakuna shida kwani wao walio kwenye field ya uigizaji ndiyo wanaojua kitu gani wanataka", aliongeza.
Sanjay Dutt amefika Arusha mapema leo akitokea Dar es salaam kwa ajili ya kuzuru mbuga za wanyama, Ngorongoro, Serengeti, mbuga ya Selou na vivutio vingine vilivyopo nchini.
Post a Comment