Header Ads

http://mtafitiblog.blogspot.com/p/blog-page.html

Shabiki wa Rooney ashindwa kuzuia hisia zake



Katika kile ambacho huenda kilitarajiwa na wengi kwamba kingetokea katika Mechi ya Everton na Gor Mahia hasa kwa uwepo wa mchezaji Wyne Rooney, shabiki mmoja alishindwa kuzuia hisia zake baada ya kuingia uawanjani na kumkumbatia Rooney.
Jamaa huyo ambae alikuwa amevaa jezi ya Manchester United hakufahamika jina lake mara moja alikimbia kutoka jukwaani na kukatiza uwanjani hadi kwa Rooney na kumkumbatia.
Katika mechi hiyo Wyne Rooney alifunga goli lake la kwanza tangu arejee Everton akitokea Manchester United sehemu aliyopata umaarufu mkubwa kutokana na mafanikio aliyoyapata.
Everton walitangulia kufunga goli la kwanza ambalo lililofungwa na Rooney kisha Medie Kagere akaisawazishia Gor Mahia kabla ya Kieran Dowell kufunga bao la pili kwa Everton
Mechi hiyo imemalizika kwa Everton kupata ushindi wa magoli 2-1 na kuwa mabingwa wa kombe lililoandaliwa na wadhamini wao wa sasa SportPesa.


No comments

Powered by Blogger.